Hazina iliyoundwa na msichana wa
kutoka Pakistan Malala Yousafzai imetangaza msaada wake wa kwanza
katika halfa iliyoandaliwa mjini New York kwa hisani ya msanii Angelina
Jolie.
Hazina hiyo ambayo iliundwa baada ya msichana
huyo kupigwa risasi kichwani na kundi la Taliban mwaka uliopita
itafadhili masomo ya wasichana 40 nchini Pakistan.Akihutubia kupitia njia ya Video kutoka London Malala alisema kuwa kuvumbuliwa kwa hazina hiyo ndio siku yake ya furaha zaidi duniani.
Hii itagharimu zaidi ya dola elfu arobaini na tano. Hazina hiyo ilianzishwa na Malala, kwa ushirikiano na wanaharakati wa elimu ya wasichana, mashirika yasiyo ya kiserikali na Umoja wa mataifa.
Kufikia sasa imekusanya dola nusu milioni, huku mchango mkubwa ukitoka kwa Angelina Jolie.
Hata hivyo bado ni wazi kuwa wasiwasi umetanda mjini Swat.
Hazina hiyo haijatangaza hadharani ni shule zipi zitakazofaidi na fedha hizo kwa hofu kuwa huenda zikashambuliwa na wanamgambo wa Taleban.
0 comments:
Post a Comment