FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

Friday, March 29, 2013

HII NDIO RIPOTI YA MAKONGO HIGH SCHOOL KUHUSU KUFELI KWA DOGO JANJA NA UTORO ULIOKITHIRI

Baada ya taarifa kuenea kuhusu uwepo wa msanii Dogo Janja nchini Afrika Kusini kwa show alizopata zilizofanyika ndani ya wiki tatu, Uongozi wa shule anayosoma ya Makongo Sekondari, umetoa taarifa kuhusu mwenendo wake pamoja na matokeo aliyopata ya kidato cha pili.
 
Michael Alfred Mbaula ambae ni Afisa taaluma amesema “mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri na alikua anashirikiana vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara yake ya mwisho kuingia darasani ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika kurudia kidato cha pili kwa sababu amefeli kwa wastani mdogo ambao usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”
 
Kuhusu kauli ya Dogo Janja kwamba juzi alipokwenda Afrika Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli kwamba aliomba ruhusa na wala ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo akitoa taarifa hata katikati ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za mziki kwa sababu Makongo ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au mbili ambazo alikua akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila kukaa miezi mitatu bila kuja shule ndio tatizo”
 
Mbaula amesema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa kupata wastani wa 27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata sifuri, Civics alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza 42, Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”

BREAKING NEWZZ .... JENGO LA GHOROFA 15 LAANGUKA

 


Taarifa lizizotufikia hivi punde zinasema kuna Jengo jipya lililokuwa linajengwa limeporomoka na kuangukia msikiti (kama inavyoonekana pichani) asubuhi hii mwendo wa saa mbili u nusu, katikati ya jiji la Dar es Salaam, inakadiriwa takribani watu 60 wamefariki dunia..

YANGA KUZINDUA TAWI JIPYA MAREKANI




TUNAPENDA KUWATANGAZIA RASMI MASHABIKI, WADAU NA WAPENZI WOTE WA TIMU YETU YA SOCCER YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB MLIOPO MAREKANI KUWA TUNAZINDUA RASMI TAWI LETU HAPA MAREKANI LITAKALO JULIKANA KAMA YOUNG AFRICANS FAMILY USA. TUNAOMBA UKIPATA TANGAZO HILI MWARIFU NA MWENZIO.

TAREHE: JUMAMOSI 03/30/2013

MAHALI: KILIMANJARO PASSION RESTAURANT

ADDRESS: 2310 PRICE AVENUE, WHEATON,MD 20902

MUDA: 4:00 PM

KWA MAWASILIANO:
ALEX KASSUWI : TEL :301 305 9685

YOUNG AFRICANS "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

BREAKING: IDADI YA MIILI ILIYOPATIKANA NA MAJERUHI MPAKA SASA BAADA YA GOROFA KUPOROMOKA LEO DAR.



Hiyo taarifa hapo chini ni ya Meya wa Ilala
Hiyo taarifa hapo chini ni ya Meya wa Ilala Jerry Silaa.
Jengo lililoanguka Dsm ijumaa ya pasaka march 29 2013 Meya on idadi ya maiti

Wednesday, March 13, 2013

MAKALA: MWIMBAJI NYOTA AMBAYE JARIBIO LA MAMA YAKE KUTOA MIMBA YAKE ILISHINDIKANA

MAKALA: MWIMBAJI NYOTA AMBAYE JARIBIO LA MAMA YAKE KUTOA MIMBA YAKE ILISHINDIKANA

Fred Hammond.                    ©chan-lo
Leo katika makala kadomole blog imeamua kukanyaga ardhi ya Marekani ambako kuna idadi kubwa ya waimbaji wa muziki wa injili ambao wanafahamika sana karibu dunia nzima na mmoja kati ya waimbaji hao ni Fred Hammond baba wa watoto wawili ambaye historia yake katika muziki wa injili inafahamika vyema. Mwimbaji huyu alizaliwa tarehe 27/12/1960 anasifika kwa upigaji mahiri wa gitaa la bass, mwimbaji pia ni mtayarishaji mzuri wa muziki ama kwa kimombo wanasema Producer.
Mwimbaji huyu anayefanya kazi chini ya lebo ya kurekodia ya Verity Records ameshiriki katika makundi mbalimbali ya gospel kama The Winans, Commissioned na kundi lake la Radical For Christ akiwa amejinyakulia tuzo za Grammy, Dove, Stellar lakini pia jina lake limewahi kupendekezwa katika tuzo mbalimbali. Katika maisha yake yote mwimbaji huyu hakuwahi kuweka hadharani siri nzito kuhusu mama yake mzazi ambaye kwasasa ni marehemu.
Kupitia katika kipindi cha mahojiano na mwimbaji mwingine mkongwe Donnie McClurkin, Fred amesema wakati mama yake akiwa na ujauzito wake alijaribu kutoa bila mafanikio.
Amesema mama yake alikwenda kliniki kwa lengo la kutoa mimba yake ambapo kwa wakati huo miaka ya 50 hadi miaka ya 60 ilikuwa ni kosa utoaji wa mimba lakini alikwenda kwa kificho na kufanikiwa kufanya kile alichokitaka kuharibu mimba hiyo ambapo aliambiwa arudi nyumbani ambako mtoto angetoka kisha angemweka kwenye begi kumrudisha hospitali, ambapo kwa mujibu wa mwimbaji huyo amesema mama yake alidhani alifanikiwa lengo lake kwakuwa alitokwa na damu na alipofika nyumbani kwa siku tatu mfululizo hakuna chochote kilichotokea. 
Akaamua kurudi tena kliniki na kuwaambia kwamba hadhani kama lengo lilifanikiwa na walipomcheki wakagundua ni kweli angali bado akiwa na mtoto hai tumboni ambapo watu hao wakamwambia siku hiyo ingewezekana kabisa kuitoa mimba hiyo na kumwambia alale kitandani tayari kwa zoezi hilo ambalo tayari kwa wakati huo watu hao walishashika vifaa kuanza kazi hata hivyo mama huyo aliamua kubadili mawazo na kuamka haraka kutoka kitandani hapo na kuvaa nguo zake kwakuwa alipata hisia ndani yake kwamba angekufa pale kitandani endapo angefanya kitendo hicho cha utoaji mimba.
Siri hii alipewa mwimbaji huyo ikiwa ni miezi mitatu kabla ya mama yake mzazi kufariki dunia, ambapo amesema ndio maana yeye hataki kuchezea huduma ya Mungu na kwamba Mungu alikuwa na makusudi naye kwani wakati mama yake alipotaka kutoa mimba yake, yeye mwenyewe (Mungu) alimwepusha na hilo na hata katika maisha aliyoishi toka wakati huo Mungu huwa anamshindia katika kila kitu. Usione Fred Hammond anaimba hiyo ni moja ya sababu inayomfanya kumpazia sauti za sifa Mungu wake aliyemuepusha na kifo.

makundi yaibuka mchakato wa kumchagua papa

Wednesday, March 13, 2013

Makundi yaibuka mchakato wa Papa

Vatican City. Dirisha limefunguliwa tayari kwa hewa safi kuingia Vatican City. Hivi ndivyo unavyoweza kuuelezea mchakato wa kumpata Papa wa 226 wa Kanisa Katoliki, unaoanza leo.
Mchakato huo unaanza rasmi saa 10.45 jioni kwa saa za Vatican (Saa 12.45 kwa saa za Afrika Mashariki) na utatanguliwa na ibada maalumu ya misa ya makadinali 115 wanaoshiriki katika uchaguzi huo.
Tayari, vumbi limeanza kutimka huku makundi makubwa matatu yakiibuka katika uchaguzi huo, unaofuatiliwa kwa karibu kote duniani na ambao unaweza kudumu hadi wiki mbili.
Makundi hayo ni pamoja na lile la makadinali wa Italia, wapatao 28 dhidi ya Wamarekani 11, wote wakiwa na malengo tofauti katika nia yao ya kuchukua wadhifa huo wa juu katika Kanisa Katoliki.
Hata hivyo, Italia ina mgawanyiko mkubwa wa vikundi vya kiitikadi miongoni mwa waumini wake, kama ilivyo kwa makadinali hao, jambo ambalo linapunguza umoja wao.
Wataliano kwa upande mwingine, wangependa kumaliza miaka 35 ya utawala wa wageni katika Vatican tangu alipoingia Papa Yohane Paul II mwaka 1978 (sasa mwenyeheri) na mfuasi wake, Benedict XVI na hivyo kurejesha miaka zaidi ya 450 ya utawala wao katika kiti hicho cha Mtakatifu Petro, wakipenda pia kudumisha mazoea ya utawala wa kirasimu katika uongozi huo.
Tofauti na miaka ya nyuma, wachambuzi wa masuala ya dini na imani, wanaona kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mwepesi zaidi kwani hakuna kadinali mwenye nyota zaidi ya wengine miongoni mwa washiriki hao 115, ambao angepewa nafasi kubwa kuibuka mshindi.
Hata hivyo, Wamarekani, taifa kubwa na tajiri duniani wanaowakilishwa na makadinali 11, imani yao ni kutaka kuupeleka nchini mwao, uongozi wa Vatican. Dhamira yao, pia inapingwa.
Hao wanadhani kuwa Marekani haiwezi kutoa kiongozi mkuu wa kanisa hilo, ambaye ataweza kukabiliana na wapinzani wa Ukristo na kuaminika kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Kundi lingine na ambalo linaweza kubadili matokeo, ni la wateule 67 wa Papa Benedict ambao ni zaidi ya nusu ya wapigakura wote.
Wao wanaelezwa kuwa mchango wao katika uchaguzi huo utakuwa mkubwa na hata kuathiri matokeo, kama watapenda kuendeleza misingi ya uongozi wake.
Pamoja na makundi hayo, kuna baadhi ya makadinali ambao kura ya maoni, imeendelea kuwabeba zaidi kabla ya uchaguzi wenyewe kuanzia leo.

Monday, March 11, 2013

FILAMU YA "RAY OF HOPE" YA KWAKE PASTOR MYAMBA YACHUKUA TUZO MARA MBILI.

Moja kati ya filamu za Swahiba yangu Pastor Myamba "Ray of Hope" imeweza kujinyakulia tuzo ya "Best Local Language Swahili" kupitia African Magic Viewers Choice Awards.Pastor Myamba amekua ni msani wa kwanza Tanzania kutengeneza filamu za Christian zenye kuonyesha umuhimu wa kumpenda Yesu kristo.

 Katika filamu hiyo waigizaji walio shiriki ni Pastor Myamba,Baby Madaha,Mzee Chilo,na Thea.Muongozaji wa Filamu hiyo Sameer Srivastava na Sajni Sirivastava.Filamu hii ilitengenezwa na kapuni ya Pilipili Entertainment na mwaka jana katika ZIFF ilishinda tuzo ya filamu bora ya Afrika Mashariki.
Kama ujapata copy yako mtu wangu wa karibu itafute ujione.

Neno La Leo: Nahofia, CCM Na Wapinzani Hawana Cha Kujifunza Kutoka Kenya!


 
 
Ndugu zangu,
Uchaguzi Mkuu wa Kenya umefuatiliwa kwa karibu sana na sisi Watanzania, ni pamoja na wanasiasa wa vyama vya siasa; Chama tawala, CCM na wapinzani.


Lakini, nahofia, kuwa hakuna ambacho vyama hivi vyetu vya siasa vitajifunza kutoka Kenya.


Ndio, pamoja na mapungufu ya hapa na pale, lakini Wakenya, kupitia Uchaguzi wao wametuachia somo kubwa sana; kuwa hata Afrika tunaweza kuendesha siasa za kistaarabu ikiwemo chaguzi Huru.


Ni kawaida kwa majirani sisi; Kenya na Tanzania, kuoneana wivu kwenye kupiga hatua kimaendeleo. Hakika ni wivu wa kimaendeleo tunaopaswa kuwa nao. Nikiri, safari hii, kama Mtanzania, nimejisikia kuwaonea wivu Wakenya kwa jinsi walivyoionyesha Afrika na Dunia kuwa nao wanaweza kuwa Taifa Kubwa; kisiasa na kiuchumi.


Mchakato ule wa mabadiliko ya Katiba yao na hata kufanya uchaguzi ule kwa amani na uwazi ni USHINDI mkubwa wa kimfumo. Ni ushindi wa Wakenya wote. Kwamba Wakenya wameujaribu mfumo mpya. Umeonyesha kuwa unafaa.


Kwa mfano, kufuatilia matokeo ya uchaguzi ule kutoka kwenye Tume yao Huru ilikuwa ni kama ‘ burudani’ ya kisiasa. Kila kitu kilikuwa kinawekwa wazi na kisayansi.


Si ajabu Wakenya waliweza kusubiri matokeo kwa juma moja bila kurushiana mawe. Na hata kama ingekuwa kusubiri kwa majuma mawili, naamini kuwa Wakenya wale wangesubiri bila kupigana, maana, wamekuwa na imani kubwa na Tume yao Huru ya Uchaguzi. Na hatukusia kule Kenya, habari ya watu ‘ kulinda kura’ wala kusimama hatua mia moja kutoka kituo cha kuhesabia kwa usiku mzima. Hiyo kazi iliachiwa Tume Huru ya Uchaguzi walioiamini.


Ndio, Wakenya wamejifunza kutokana na ujinga wa wanasiasa wao uliopelekea vurugu za baada ya Uchaguzi wa mwaka 2007. Wengi walikufa na wengine kupoteza makazi na mali zao. Wakaanza haraka mchakato wa kuifanyia marekebisho makubwa Katiba yao. Wakapata Katiba Mpya 2010. Wakenya wale wametumia gharama kubwa kwa kuitafuta amani yao. Kimsingi, tangu 2010, Wakenya wamekuwa ‘ wakiangushiwa mabomu ya ujumbe wa amani’- Ni kila kukicha.


Serikali yao imetumia fedha nyingi sana kufikisha ujumbe wa amani kwa Wakenya. Sasa wanavuna walichopanda; kuwa na chaguzi huru za amani na utulivu. Na walichokitafuta Wakenya kwa gharama kubwa, kwa maana ya amani, sisi Watanzania tulikuwa nayo, sasa tunaipoteza wenyewe ili baadae tuanze kugharamia kuitafuta. Ni ulimbukeni.


Kwa kupitia Katiba yao ya sasa Wakenya wameweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ukabila. Kwa namna gani?


Ona kwenye kugombea Urais; mgombea lazima afikishe asilimia 50+1 ( Asilimia 50 na kura moja) ili aweze kutangazwa mshindi. Mgombea pia lazima akubalike kwa asilimia 25 ya Counties zote ( Majimbo yote).

Sasa basi, kwa Kenya, Wakikuyu ni asilimia 23 ya Wakenya. Wajaluo asilimia 11.

Nyingine zilizobaki ni za makabila mengine madogo madogo. Hivyo, ili mgombea ushinde zaidi ya asilimia 50 una lazima ya kukubalika kwenye maeneo mengine nje ya wigo wa kabila lako. Kwamba kula za Wakikuyu pekee kwa Uhuru Kenyatta zisingetosha, vivyo hivyo kwa Odinga.


Utaratibu huo unaua ukabila na kujenga vema misingi ya Utaifa. Hata kama itachukua muda kufika mbali zaidi katika hilo lakini Wakenya wameanza kuondokana na ukabila kwenye siasa zao, kwa kupitia Katiba.


Kwa mantiki hiyo hiyo, Watanzania tungeweza kabisa kuondokana na siasa za udini kwa kuweka, kwenye Katiba yetu ijayo sharti la mgombea Urais kushinda kwa asilimia 50+1 ( Asilimia 50 jumlisha kura 1). Hilo lingewafanya wanasiasa wetu wenye kuwania Urais na vyama vyao pia ‘ Kutia akili’.



Maana ingekuwa na tafsiri moja kuu; kuwa mgombea na chama chenye kuendekeza udini kisingekuwa na nafasi ya kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala nafasi ya kushika dola. Maana, hakuna dini hapa Tanzania yenye idadi ya waumini wanaovuka asilimia 50 ya jumla ya Watanzania.


Kwa maana, hiyo, muarobaini wa kumalizana na udini uko kwenye Katiba ijayo, kama tuna nia ya dhati ya kutoka hapa tulipo. Vinginevyo, udini huu tunaosema kuwa ni tatizo tutakuwa tunaulea wenyewe.



Hata tatizo la siasa za ukanda nalo litapotea, maana, hakutakuwa na mgombea au chama kitakachoweza kushinda na kutoa Urais kwa kuegemea kura za kikanda. Hakuna kanda itakayovuka peke yake asilimia 50 ya kura zote. Chama na mgombea kitahitaji kuungwa mkono na wapiga kura wa kanda hata zilizo nje ya anakotoka mgombea Urais.



Vinginevyo, kama alivyotamka Uhuru Kenyatta kwenye hotuba yake nzuri iliyojaa utaifa hivi majuzi, kuwa katika uchaguzi waliofanya, kila kura ilikuwa ina umuhimu. Hivyo, kila kabila lilikuwa na umuhimu. Na Uhuru Kenyatta akaweka wazi anachotaka Serikali yake kwa kushirikiana na Wakenya kufanya ili kuitoa Kenya hapo ilipo na kwenda mbele.



Kenyatat alimalizia na maneno matatu; Forward, Foward. Foward!- Kusonga mbele!


Ndio, Wakenya wameamua; KENYA KWANZA!

And really, The Kenyans are coming, Big Time!

Ni ukweli, Wakenya wanakuja. Kisiasa na kiuchumi. Sisi hatujajipanga na hatutaki kujipanga kwa dhati. CCM na wapinzani, na hata media yetu, kama kawaida, tumerudi kwenye kucheza ‘ Kiduku’ chetu. Hatuna cha kujifunza kutoka Kenya. Tumerudi kwenye mambo yetu ya hovyo hovyo; ni Siasa za Mwembe Yanga na Viwanja Vya Jangwani. Siasa za kupigana vijembe. Siasa za reja-reja- Retail politics.


CCM na wapinzani ni kama vile wapenzi wa soka. Wanaangalia kila siku soka la majuu. Wataongea sana kuhusu soka la majuu lilivyo bora.


Lakini, wakirudi kwenye soka lao, ni yale yale, hawana cha kujifunza na hawataki kujifunza. Ni madudu kwenye kuendesha vilabu na hata kufikia kununua mechi kwa kuhonga marefa, wachezaji na viongozi. Ukisema nini hiki?


Utajibiwa; “Wewe Bongo mpira pesa bwana!” “Mpira fitna!” Ni kama majibu ya wanasiasa, iwe wa CCM au vyama vya upinzani. Nao watakwambia; “Wewe, Bongo siasa pesa bwana!” “ Siasa mizengwe na fitna!”


Naam, nahofia, kuwa CCM na wapinzani hawana cha kujifunza kutoka Kenya!


Maggid Mjengwa,

Thursday, March 7, 2013

ASKOFU BANDIA AJIPENYEZA MKUTANO WA MAKADINALI


Askofu bandia amefanikiwa kujipenyeza na kuingia kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya.

Askofu huyo bandia, Ralph Napierski ambaye ni mzawa wa Ujerumani alifanikiwa kujipenyeza na kusalimiana kisha kupiga picha za kumbukumbu na baadhi ya makadinali waliopo kwenye mkutano huo bila kugundulika.

Uzamiaji wake ambao ulileta mashaka kuhusu uimara wa usalama eneo hilo wanapokutana makadinali 103, ambao wamekusajika kwenye Makao Makuu ya Kanisa Katoliki kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya, huku wengine 12 wakiwa hawajawasili.

Katika mkutano huo, Kadinali wa juu kutoka Uingereza, Cormac Murphy O'Connor pia anahudhuria.


Mtu aliyejifanya Kardinali wa Kanisa Katoliki, Ralph Napierski (kushoto) akisalimiana na Kardinali Sergio Sebiastiana. Napierski alikamatwa akijaribu kuingia kwenye mkutano wa makardinali unaoendelea Vatican

Napierski alionekana akisalimiana na Kadinali Sergio Sebiastiana nje ya ukumbi wa Papa Paul VI akiwa hajatambua kuwa siyo miongoni mwa wenzake, huku akiwa amezungukwa na makasisi wengine wa kanisa hilo ambao pia hawakuweza kutambua.

Walinzi wa kundi la Swiss Guars linaloshughulika na ulinzi wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican, walimbaini kuwa siyo miongoni mwa wahusika kutokana na vazi lake alilofunga kiunoni, ambalo siyo sahihi bali ulikuwa ni mtandio uliokunjwa vizuri.

Pamoja na vazi hilo la rangi ya zambarau kutokuwa sahihi, pia kofia aliyokuwa ameivaa haikuwa miongoni mwa zile zinazotambulika kuvaliwa na viongozi wa kanisa hilo.

Tofauti nyingine iliyobainika ni ufupi wa kanzu yake na rozari aliyovaa haikuwa halisi, kwa kuwa ilikuwa ni fupi kuliko wanazotumia viongozi wa kanisa hilo.

Kabla ya kubainika, Napierski alijitambulisha kwa waandishi wa habari kwamba jina lake ni Basilius ni miongoni mwa wawakilishi wa Kanisa la Orthodox kutoka Italia.

Awali, kulikuwa na taarifa kwamba aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Kanisa Katoliki limefanya “Kosa kubwa” kwa kuwaruhusu makasisi wanaotuhumiwa kwa makosa ya ngono kubadilishwa kutoka maeneo yao ya awali na kupelekwa kwingine, kuficha kashfa zao badala ya kuzishughulikia.

Mtuhumiw ahuyo ambaye baada ya kubainika aliondolewa eneo hilo, anaongoza tovuti ambayo aliitumia kujitambulisha kwamba yeye ni kasisi kupitia Shirika la Kikatoliki la Corpus Dei, huku akiwa amevaa mavazi ya kikasisi na kujidhihirisha kama “Mtumwa na Nabii kama Mtakatifu Paul”.

Msemaji wa Kanisa Katoliki mjini Vatican, Federico Lombardi alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa yoyote na muda wote alikuwa akishughulika katika mkutano

Source:mwananchi.co.tz
You might also like: