Monday, April 15, 2013

MTOTO WA MIAKA 8 ALIYEFUNGA NDOA NA MWANAMKE WA MIAKA 61 WANAENDELEA VIZURI NA MAISHA YA NDOA!


 Ndoa hii iliyofungwa wiki iliyopita nchini ya Afrika Kusini kati ya mtoto huyo wa kiume mwenye miaka 8 Sanele Masilela na mwanamke wa miaka 61 Helen Shabangu na kuzua gumzo dunia nzima.

 Walipokuwa ndani ya suti na shela
 Katika mavazi ya kimila...inasemekana ndoa hiyo ilifungwa ili kutiii mila maana mzimu wa babu yake ulimuomba aoe kwa niaba ya babu yake ambae ni marehemu.
Mtoto Senele amepewa jina la marehemu  babu yake anasema babu yake alikuwa akisikitika kuwa hakuwahi kufunga a white wedding hivyo akamuomba afunge hiyo ndoa kwa niaba yake.Na yeye akamchagua Hellen kwani ni rafiki yake.Hellen ni mke wa mtu na pia ni mama wa watoto watano.
 Maisha yanaendelea,Mtoto Sanele akipata chakula nyumbani kwa Hellen!
 Sanele akiwa amerudi katika maisha yake ya kawaida akicheza mpira na wenzake.
 Family inafurahi kuweza kutimiza maombi ya mizimu.Hellen anaishi kwake na mumewe na watoto kama kawaida japo amefunga ndoa na mtoto Sanele.
Dunia na vijimbambo!

0 comments:

Post a Comment