Papa Francis akizungumza na umati wa watu katika uwanja wa Mtakatifu Peter jijini Vatican, kwenye salamu zake 'kwa jiji na ulimwengu.' "Urbi et Orbi". © Reuters/Stefano Rellandini |
Salamu za mara ya kwanza kutoka kibaraza cha Mtakatifu Basilica mjini
Vatican, eneo ambalo Papa Francis alisimama kwa mara ya kwanza kutoa
salamu za pasaka, ndipo hapo ambapo Papa aliombea amani katika bara la
Asia, hususan kwa taifa la Korea, kutokana na kuwa katika hatihati ya
kuingia vitani baina ya mataifa hayo mawili ya kusini na kaskazini.
"Amani kwa Asia, hasahasa ukanda wa Korea, naomba kutokuelewana kote
kugeuke na roho ya mapatano ihuishwe na kuelewana" Papa Francis alianza
kuzungumza, akieleza kwa lugha ya Kiitalia, akisalimia watu zaidi ya
laki mbili na nusu, katika salamu yake ya pasaka kwa mara ya kwanza
akiwa Papa.
Katika salamu hiyo, pia aliomba Yesu awaguse watu wabadili chuki kuwa
upendo, kisasi kuwa kusameheana na vita kuwa amani, shirika la habari la
Reuters limeripoti.
Ujumbe huu wa Papa umekuja wakati ambao uhusiano wa Korea Kaskazini na
Marekani ukiwa katika hali ya mashaka zaidi. Mnamo mwezi uliopita, taifa
hilo la Pacific lilisema kuwa linasitisha makubaliano yake ya
amaniambayo yalisainiwa mwaka 1953, licha ya kwamba nchi hizo mbili
zimekuwa katika hali ya kutaka kupigana kwa kipindi cha miaka 60 sasa.
Viongozi mbalimbali wakisaini mkataba wa makubaliano ya amani baina ya nchi za Korea. |
Korea Kaskazini pia imekuwa ikirusha madongo na kujitamba mbele ya
Marekani, ikisema kuwa ina silaha za nyuklia ambazo zina uwezo wa
kushambulia mbele ya sheria za Umoja wa Mataifa, katika kujibu hilo,
Marekani wao wakatuma nchini Korea Kusini ndege za kivita aina ya F-22,
zenye uwezo wa kutoonekana kwenye rada, ili kufanya nao mazoezi ya
pamoja na kujiweka tayari kwa chochote ambacho Korea Kaskazini itafanya.
0 comments:
Post a Comment