Mbunge wa
Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amemlipua kigogo mmoja wa
juu wa CCM (jina tunalihifadhi kwa kuwa hakupatikana kujibu tuhuma
hizo), kuwa ndiye kinara wa biashara haramu ya pembe za ndovu na
utoroshaji wa wanyama nchi za nje.
Akihutubia
mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa jana, Mchungaji
Msigwa alisema anashangaa Serikali ya CCM kushindwa kumchukulia hatua.
Mchungaji Msigwa alidai kuwa tembo wapatao 75 wamekuwa wanauawa kila siku kutokana na tatizo hilo kufumbiwa macho na Serikali.
Alidai kuwa
pamoja na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige
kujiuzulu mwaka jana kutokana na kashfa ya kutorosha twiga, Serikali
ilitakiwa kuwafuatilia wahusika wote.
“Kinara wa biashara haramu ya uuzaji wa pembe za ndovu anajulikana, sasa inakuwaje Serikali inashindwa kumkamata?” alisema Msigwa na kuahidi kulipua mabomu zaidi atakaporudi bungeni kwa maelezo kuwa anao ushahidi wa suala hilo.

Huo ulikuwa
mkutano wa mwendelezo wa wabunge wa Chadema waliosimamishwa kuhudhuria
vikao vya Bunge kuwapasha wananchi sababu ya kuchukuliwa hatua hiyo.
Wabunge hao walisimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje ya ukumbi, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu. Wabunge waliosimamishwa pamoja na Lissu ni Godbless Lema (Arusha Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Ezekiah Wenje (Mwanza Mjini) na Msigwa.

Hata hivyo, Lema na Lissu hawakuwapo katika mkutano huo wa jana ambao pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.
Mnyika kutoa hoja binafsi
Katika mkutano huo, Mnyika aligawa fomu kwa wananchi kuomba aungwe mkono wakati atakapotoa hoja binafsi bungeni juu ya mfumuko wa bei na umaskini nchini.
Mbunge huyo alisema wananchi wanakabiliwa na maisha magumu kutokana na hali mbaya ya uchumi.
“Napata
uchungu ninavyoona Watanzania wakiishi maisha magumu kwa hiyo naandaa
hoja binafsi ya kuwasilisha bungeni ili umma uelewe umuhimu wa suala
hili,” alisema Mnyika na kuongeza kwamba atagawa fomu hizo kila
atakapohutubia mikutano ya hadhara.
Dk Slaa na Usalama wa Taifa
Katika mkutano huo, Dk Slaa alidai kuwa maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wamegawanyika kutokana na makundi ya wanaotaka kuwania Urais mwaka 2015 kupitia CCM.
Dk Slaa na Usalama wa Taifa
Katika mkutano huo, Dk Slaa alidai kuwa maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa wamegawanyika kutokana na makundi ya wanaotaka kuwania Urais mwaka 2015 kupitia CCM.
Dk Slaa alisema mgawanyiko huo ndiyo chanzo cha siri nyingi za idara hiyo kuvuja.
Aliwatuhumu baadhi ya wanachama wa CCM akidai kuwa wamekuwa wakiwavuta baadhi ya maofisa katika idara yao ili kuwasaidia kwenye harakati zao.
Aliwatuhumu baadhi ya wanachama wa CCM akidai kuwa wamekuwa wakiwavuta baadhi ya maofisa katika idara yao ili kuwasaidia kwenye harakati zao.
0 comments:
Post a Comment