Wiki
iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra
pichani.Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es
salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka
takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata
watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote
wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata
kuchanwa na viwembe.
Mwezi
wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa
wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata
akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea
akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa
akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate
nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma
akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo
kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta
akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.
Kiukweli
aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na
kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7
zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa
Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya
Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana
baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana
akavimba na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa
katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania
maisha yake.
Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.
Usiku wa kuamkia jumanne ya tarehe 10
Nasra akaaga dunia.Ilikuwa ni huzuni sana jinsi alivyoteseka na namna
mazingira ya kifo chake kilivyotokea.Tulikuwa na matumaini kuwa angeweza
kupona maana dakika za mwisho alikuwa anaongea japo kwa shida.
Tunaomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nasra mahala pema peponi,Amina.
0 comments:
Post a Comment