Tuesday, April 16, 2013

JUSTIN BIEBER ANAPATA USINGIZI KWA KUSIKILIZA NENO LA MUNGU


Justin Bieber akiimba jijini Manchester mapema mwaka huu. Picha ©Reuters/Phil Noble.
Mchungaji Judah Smith anayeongoza kanisa la City church katika mji wa Seattle huko Washington nchini Marekani ameweka wazi kwamba huwa anawasiliana na mwimbaji nyota wa muziki wa nje ya kanisa Justin Bieber(19) katika kumsaidia usomaji wa neno la Mungu.

Mchungaji Judah ambaye ndiye mchungaji wa kijana huyo, amesema yeye na mwimbaji huyo wamekuwa wakiwasiliana na kushirikishana maandiko katika shughuli za kila siku, mwimbaji huyo amekuwa akisoma neno la Mungu na kusikiliza mafundisho yake ya kiroho kwa njia ya kanda mara nyingi nyakati za usiku ambayo humfanya kulala usingizi mzuri kama mtoto mdogo.

Mchungaji Smith ameweka wazi hivi karibuni wakati anazungumza na E! News kuhusu kukutana na mwimbaji huyo pamoja na mama yake aitwaye Pattie Mallette wakati walipohudhuria kongamano ambalo mchungaji huyo alikuwa akifundisha miaka ya michache iliyopita.

Mchungaji Smith amesema mafundisho yake ya kiroho yanamsaidia mwimbaji huyo kulala kama mtoto na,amesema alipokutana naye kitu cha kwanza Bieber alimuuliza swali mchungaji huyo unakumbuka ulikutana nami, mchungaji akasema hapana katika mazungumzo hayo na E! News ambapo mwimbaji huyo akamwambia unanifanya nilale wakati wa usiku.

Hivi karibuni mchungaji Smith alizindua kitabu kiitwacho "Jesus Is" ambacho mwimbaji huyo alikitangaza kupitia akaunti yake ya Twitter ambako ana mashabiki na marafiki zaidi ya milioni wanaomfatilia, ambapo mapema mwaka huu mchungaji huyo alisema hana chochote kwa mwimbaji huyo zaidi ya kuahidi kufanya awezalo katika kumtia moyo kwakuwa ni kijana wa kipekee jambo ambalo aliliweka wazi wakati alipoonekana kwenye runinga ya Fox mapema mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment