8:38 AM
Msiba New Jersey
Kuna kijana amefariki New
Jersey, USA. Kijana aliyefariki alinajulikana kwa jina la Adolf, Brian
au Tadeous Rwekagende. Alikua anasema alisoma Tambaza na alikua na mdogo
wake anaitwa Rodrick Rwekagende ambaye naye alikua anaishi Texas. Ila
cha kusikitisha ni kuwa huyo mdogo wake alisema alifariki mwaka jana
mwezi wa nne (Tanzania).
Adolf alikua anasema baba yake na mama yake walifariki yeye na mdogo
wake huyo wakiwa wadogo. Sasa yeye alikulia kwa mjomba wake. Juzi Adolf
alipata massive stroke na kulazwa st Barnabas hospital, Livingston, NJ
na kufariki. Mpaka sasa hivi kuna watu wametafuta ndugu zake na kumpata
mjomba wake mmoja huko Bukoba vijijini. Hatukuweza kupata ndugu wa
karibu hapa marekani na mpaka sasa hivi maiti yake ipo hospital haijawa
claimed. Hivyo kama binadamu tumeamua kujichangisha ili tuweze kupeleka
mwili wa mwezetu Tanzania kwa mazishi. Gharama za kuzika huku na
kusafirisha kupeleka Tanzania ni karibu sawasawa tu hivyo tunaona ni
bora akapumzike na ndugu zake Tanzania.
Hivyo tunaomba mtupostie kwenye blog zenu hili tangazo liwafikie
watanzania watakaopenda kumsaidia ili apelekwe Tanzania tutashukuru
sana. Tumefungua mahali pa kuchangisha hela http://www.donationto.com/adolfsendhomecost au kama mtu anatumia paypal account ni adolffuneralcost@gmail.com.
Tutawapa majina ya watu watakaokua kwenye kamati ya kukusanya hela mara
tutakapomaliza kikao tunachotegemea kufanyika Jumamosi. na hela zote
zitaonyeshwa zilivyotumika kama zipo extra zitapelekwa huko kwa wajomba
zake Bukoba.
Na kama kuna mtu ana picha yake basi mtutumie kwa sababu hakuna mtu
aliye na picha yake. ID yake ipo hospital hawawezi kumpa mtu mpaka
wakishajua nani anachukua mwili na mahali alipokua anaishi hawaruhusu
mtu kuingia kwa sasa mpaka wakishajua mazishi ni wapi au ndugu wa karibu
ni wapi. Hivyo hamna mtu ana picha yake..
Please sisi hapa tunajitahidi ili azikwe kama ubinadamu hivyo huu
sio muda wa kuanza kuuliza maswali kwa nini hiki wala kile...Kwa vile
hata sisi tuna maswali mengi na hakuna mtu mweye
jibu....Tunachojua ni
kuwa alipata massive stroke na amefariki na hakuna ndugu yake wa karibu
huku marekani.
Tunatanguliza shukurani na pia kama blog yako hupost mambo ya habari
tunaomba utusaidie kuforward hii email kwa watu wengine...Kuna wazee
wako NY kama wakikukubali kushughulikia huu msiba tutawatangazia na
kuwapa information mpya. Na hela zitakazopatikana zitahamishiwa kwenye
fund yeyote watakayofungua kama wataamua kufungua mpya au wataamua
kuendelea na hi hii. Tunachotaka ni kusafirisha kijana wa watu Tanzania
kwa sababu sasa hivi hilo ndio lengo letu....na hakuna mtu yeyote
aliyesema kitu chochote hivyo kama kikao kikifanyika basi tutawaeleza
linaloendelea.
Nitajitahidi kuupdate kinachoendelea katika twitter handle yangu @swahilimom
Regards,
Pauline
0 comments:
Post a Comment