FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

FOR MORE INFORMATION ON.

ADVERTISING YOUR BUSINESS AND MARKETING !! CONTACT.+255 765 326 668

Tuesday, April 30, 2013

PICHA ZA UCHI ZA DENTI WA CHUO KIKUU HAPA NCHINI ZAVUJA MITANDAONI





 MDADA MWENYEWE NI HUYU.



DENT mmoja katika Chuo Kikuu kimojawapo hapa nchini amepiga picha zisizo na maadili akiwa na njemba wake katika visiwa vya Zanzibar.


Mwanafunzi huyo alionekana kutumia muda wa masomo kufanya mambo yake hayo, na kilichowashangaza wengi kile kitendo cha yeye kutoka DODOMA mpaka ZANZIBAR ili kutimiza haja zake katika kipindi ambacho wenzake walikuwa katika masomo..


DADA HUYO NA NJEMBA WAKE WAKIENDELEA KULA RAHA.....




MAMA ZITO ADAI WANATAKA KUMUUA.

SHIDA Salum ambaye ni mama mzazi wa mwanasiasa machachari ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema kuna watu wanataka kumuua.



                                                  Mama Shida Salum.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita, Shida alisema Aprili 19, mwaka huu, saa moja na nusu katika Ghorofa la NSSF maeneo ya Tabata Bima, hawezi kuisahau kwa kuwa ndiyo siku ambayo majambazi walimvamia wakiwa na bastola.
Akisimulia mkasa huo Shida alikuwa na haya ya kusema:
“Majambazi hayo yaliyonivamia siyajui lakini mmoja wao huwa namuona. Kabla hawajaja walinipigia simu wakaniambia wana shida na mimi lakini hatukupanga namna ya kuonana.
Uwazi: Sasa walipofika nyumbani kwako, uliwakaribishaje?
Shida: Walipofika walivamia na kufanikiwa kuingia sebuleni.
Uwazi: Baada ya kuingia ikawaje?
Shida: Cha kwanza walichotaka ni laptop (Kompyuta mpakato), flash na simu zangu.
Uwazi: Uliwapa?
Shida: Baada ya kutoa amri hiyo niliwajibu kuwa kompyuta iko ofisini na simu niliwaambia ziko kwenye chaji.
Uwazi: Baada ya hapo ikawaje?
Shida: Mmoja wa majambazi hayo alinionyesha bastola kuwa kama sijatii hayo wanayoniambia basi watanifanya kitu kibaya,   ndipo nikamuita kijana wangu aitwaye Mtana aende chumbani kuchukua simu zangu niwape.
Uwazi: Ikawaje?
Shida: Niligundua kuwa Mtana alikuwa anasikia amri zilizokuwa zikitolewa na majambazi hayo, hivyo alipiga kelele kuomba msaada kwa wananchi.
Uwazi: Majambazi wakafanya nini?
Shida: Waliposikia kelele walikimbilia nje, wakaingia ndani ya gari lao ambalo namba zake zisijui, wakatoweka.
Uwazi: Pole sana.
Shida: Pamoja na purukushani hizo namshukuru Mungu sana kwa kuwa hawakunidhuru na hawakufanikiwa kuchukua chochote.
Uwazi lilitinga nyumbani kwa mama huyo na kukuta ulinzi ukiwa umeimarishwa ambapo sasa kuna askari wenye bunduki.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, majambazi hayo yalifanikiwa kuingia ndani baada ya mlinzi aliyekuwepo zamu kwenda kubadili nguo za kiraia ili avae za kiaskari.
“Tukio lilikuwa la haraka sana, wakati askari huyo anatoka kwenye kibanda cha kubadilishia nguo ndipo na wale majambazi walipokuwa wakitoka ndani na kuingia kwenye gari lao,” kilisema chanzo.
Waandishi wetu walimtafuta kiongozi wa walinzi wanaolinda nyumbani kwa mama huyo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Ngosha na alipoulizwa kuhusu sakata la kuvamiwa alikiri kulifahamu.
“Baada ya tukio lile tumeimarisha ulinzi ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao. Sasa tumeweka askari wenye bunduki na tunaamini tukio kama hilo halitajirudia,” alisema Ngosha.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minagi alikiri kutokea kwa tukio hilo.
“Nina taarifa ya tukio hilo na tunaendelea na upelelezi kuwasaka majambazi hao, wananchi waondoe hofu.” alisema Kamanda Minagi.

MKURUGENZI IDARA YA MAELEZO ASSAH MWAMBENE AJARIBU UDIKTETA KAMA ULE WA MWANAHALISI DHIDHI YA TWITTER




Majuzi tumeshudhudia jinsi Mbunge wa CCM Peter Serukamba akitukana tusi baya kabisa huko Bungeni. Siku chache baadaye tukashuhudia ubabe wa kipuuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha dhidi ya wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu na Mbunge wa Chadema Godbless Lema.

Kabla kumbukumbu hizo mbaya hazijaondoka vichwani mwetu amejitokeza mtendaji mwingine wa serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo Assah Mwambene, kuendeleza madudu yaleyale yanayozidi kuthibiths kuwa kuna ombwe kubwa la uongozi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.

Jana kulikuwa na mjadala ulioanza tangu asubuhi huko Twitter kuhusu utendaji kazi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Mjadala huo ulielemea zaidi kwenye jinsi taasisi hiyo inavyofanya kazi kwa kuipendelea CCM huku matishio halisi ya usalama wa taifa letu yakipuuzwa.

Kama mwananchi wa kawaida na mtumiaji wa kila siku wa Twitter nilijumuika katika mjadala huo.Kimsingi, hakukuwa na matusi wala maneno ya kuudhi bali mjadala uliotawaliwa na busara na jitihada za kushawishi mabadiliko ya uendaji kazi wa TISS.

Ghafla akajitokeza Bwana Mwambene, na kuanza kuhoji kwa nini tunaijadili TISS kiholela. Nikajaribu kumfahamisha kuwa Twitter haipo chini ya Idara ya Maelezo, na ni mtandao wa jamii ambao unaruhusu watumiaji kutoa mwazo yao angalau kwa ustaarabu.

Badala ya kuzingatia ushauri huo,Bwana Mwambene akanigeukia mie akidai inashangaza kuizungumzia TISS ambayo ilinifukuza kazi (kwa mujibu wa maelezo yake).

@isongole: @chahali jamani kama mmekosa story za kuongea ebu kaeni kimya mimi. najua baadhi yenu mlivyofukuzwa kazi mnataka ndo iwe hoja hapa

Akaendelea 

@isongole: @Chahali ukifika kuitukana taasisi iliyokufukuza kwa makosa tunayoyajua unataka tusemeje kwenye mtandao hii ndugu yangu.

Sasa utoto huu wa kutishiana vitu ukifanywa na mtu wa kawaida sawa, lakini unapofanywa na mtu aliyeteuliwa na Rais kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali inatia doa hata huyo Rais aliyefanya uteuzi huo.Kama mpuuzi huyu anajua SIRI iliyopelekea 'kunifukuzisha kazi' (kwa mujibu wake) kwanini asiiweke bayana badala ya 'kunitishia mtu mzima nyau'?


Hawa ndio wapuuzi waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi nyeti kabisa.Hawajui tofauti ya lugha ya malumbano mtaani na lugha ya kiofisi.


(Lakini kwa upande mwingine, tutegemee nini kwa mtu aliyeonyesha u-kichwapanzi kama huu? 
Katika hali isiyoeleweka, Mkurugenzi wa Habari na Maelezo Ndg. Asah Mwambene alijikuta akitoboa siri hadharani, either kwa makusudi au bila kukusudia aliposema Mh. Zitto alimtahadharisha asiwe na urafiki na watu kama Mkurugenzi wa gazeti la MwanaHalisi Ndg Saed Kubenea isije kumharibia kazi. Asah alisema Zitto alimpa ushauri huo muda mfupi tu mara baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo kutoka kwa Clement Mshana ambaye amekwenda TBC alipokwenda bungeni Dodoma kujitambulisha kwa Waheshimiwa wabunge. )

Kwa upeo wake finyu, mteuliwa huyu wa Rais alidhani kuwa porojo zake kuwa "nilifukuzwa TISS"  zingenitisha nisiendelee kujadili masuala muhimu yanayohusu mustakabali wa taasisi hiyo na taifa kwa ujumla.

Sijui kama alitumwa na serikali kuja kufanya vitisho hivyo huko Twitter au ni kimbelembele tu cha kulind ajira yake inayopeleka mkono wake kinywani, lakini kilicho wazi ni kuwa Bwana Mwambene alitaka kuigeuza Twitter kama chombo cha habari cha Tanzania kinachofanya kazi chini ya uangalizi mkali wa serikali kupitia Idara ya Maelezo inayoongozwa na Mwambene.

Sipendi kuzungumzia maisha yangu ya zaidi ya miaka 10 kama mtumishi wa TISS (ambapo nilianza kutoka ngazi ya chini kabisa hadi kufikia ukuu wa kanda ya kiusalama). Lakini tofauti na madai ya Bwana Mwambene kuwa nilifukuzwa kazi kwa makosa anayoyajua, nililazimika kuachana na taasisi hiyo kutokana na kuandamwa mara kwa mara kwa sababu ya makala nilizokuwa nikiandika kwenye magazeti ya Kulikoni na Mtanzania na baadaye Raia Mwema (baada ya kuja masomoni huku Uingereza).

Niseme ilifika mahala kuwa ajira yangu ndani ya taasisi hiyo ilikuwa haiwezekaniki kutokana na tuhuma na hisia kuwa makala zangu zilikuwa zikiwatumikia wapinzani wa chama tawala na hisia kuwa nilikuwa nikitumikia 'taasisi zaidi ya TISS' (kosa ambalo kisheria ni uhaini).

Mwezi Oktoba mwaka 2006 nilipigiwa simu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TISS Bwana Jack Zoka akihoji kama mie bado ni mtumishi wa serikali ya Tanzania au la, na kuniamuru niache kuandika makala za siasa hususan zile zinazoikosoa CCM. Tukio hilo lililotokea siku chache baada ya mie kuandika makala iliyokuwa ikimkosoa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa katika jitihada zake za ku-lobby wabunge wa CCM wasijadili ishu ya Richmond. Miaka miwili baadaye, ishu hiyohiyo iliyomfanya Zoka anipigie simu ilipelekea Lowassa kulazimika kujiuzulu.

Siandiki makala hii kumshawishi Mwambene au mtu yeyote yule kuwa uamuzi wangu kuachana na TISS ulitokana na unyanyasaji dhidi yangu kwa sababu tu ya maoni yangu ya kisiasa (political opinions). Ninajivunia nilivyolitumikia taifa langu wakati huo na ninavyoendelea kulitumikia hivi sasa kupitia makala zangu.

Sijisikii aibu kutuhumiwa kuwa nilifukuzwa kazi kwa vile tu nilisimami kwenye haki.Wa kujisikia aibu angekuwa marehemu Daudi Balali (kama ni marehemu kweli) aliyekwapua mamilioni ya fedha na 'kuingia mitini' kisha tukaambiwa amefariki. Sijisikii aibu kwa vile mie si mmoja ya watumishi wa TISS ambao walitajwa kuhusiska na ufisadi wa EPA lakini hawajachukuliwa hatua hadi leo.

Kilichonikera ni mawazo ya kale ya Bwana Mwambene kudhani kuwa Twitter inaweza kuzibwa mdomo kama walivyofanya kwa gazeti la Mwanahalisi ambalo kosa lake pekee ni habari iliyomtaja Afisa Usalama wa Taifa aliyehusika na utekaji na uteswaji wa Dokta Ulimboka 

Talking about Mwanahalisi, hiki ndicho alichosema Bwana Mwambene 

@isongole: @Chahali  Mwanahalisi ilifinguwa nikiwa Mambo ya Nje lakini hata ningekuwepo ningewafungia maana walipita mipaka ya taaluma ya uandishi

Huwezi kuamini kuwa kauli hii inatoka kwa mtu ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari. Mwambene anafahamu fika kuwa laiti gazeti la Mwanahalisi lingekuwa limekiuka maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari za uchochezi au kashfa basi sehemu mwafaka kwa serikali na gazeti hilo kupata haki ilikuwa mahakamani.

Mwanahalisi lilifungiwa kwa sababu moja tu: kuliziba mdomo lisiweke hadharani mkakati dhalimu unaoendelea wa kuteka na kung'oa kucha kila anayeonekana tishio kwa utawala wa kifisadi.

Majuzi walituma wazembe flani kujaribu kunidhuru (naamini bado wanaendelea na mkakati huo dhalimu ambao nina imani hautofanikiwa). Sasa wameafikia hatua ya kumtuma Msemaji wa Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo Bwana Assah Mwambene ajaribu kutuziba mdomo hadi kwenye mitandao ya kijamii.

Halafu Rais Kikwete anasema nchi haijamshinda ilhali watendaji wake wanafanya mabo ya kipuuzi kana kwamba ni wahuni wa vijiweni. Does it make any sense kwa Msemaji wa Serikali kuingilia maongezi ya kawaida tu ya wananchi huko Twitter na kuwalazimisha waache kuongelea 'mambo nyeti.'? Huu sio udiktrata bali upuuzi wa hali ya juu


Nimalizie makala hii kwa kumtahadharisha Mwambene kuwa hakuantawala iliyokuwa na nguvu za kutisha huku ikitumia mashuishushu kial kona kama USSR (Muungano wa Jamuhuri za Kisosahalisti za Urusi). Pamoja na nguvu kubwa za taasisi yake ya ushushushu ya KGB, haikuwezekana kuzuwia kuporomoka kwa utawala wa USSR na ukomunisti wa Ulaya Mashariki kwa ujumla.

Kuna siku CCM itaondoka madarakani, na ni wakati huo ambapo watu kama Mwambene watakuwa wanahaha kutafuta sehemu za kujificha. Huo utakuwa ni uhuru wa pili kwa wote wanaonyanyaswa sasa kwa vile tu si miongoni mwa watawala wachache, sambamba na akina sie tunaopiga kelele zinazotishia kutia mchanga kwenye keki ya taifa inayotafunwa na mafisadi.



Time will tell!

Mourinho na vijana wake kuvuna nini leo Ulaya?


http://www.footballtarget.com/wp-content/uploads/2012/11/real-madrid-vs-borussia-dortmund-match-preview-champions-league.jpg
KOCHA Jose Mourinho na vijana wake wa Real Madrid leo wana kibarua kizito cha kuudhibitishia dunia kwamba soka lina maajabu yake watakapowakaribisha Borussia Dortmund nyumbani kwao, Santiago Bernabeu katika nusu fainali ya marudiano wakiwa na deni la kipigo cha mabao 4-1 walichopewa ugenini.
Mourinho na vijana wake walichezea kichapo cha mabao 4-1 ugenini nchini Ujerumani katika pambano la kwanza la Nusu Fainali ya michuano hiyo na hivyo leo watalazimika kulipa kisasi ili  kutinga fainali na kusaka taji la 10 na la kwanza tangu mwaka 2002.

Madrid watahitajika kushinda mabao 3-0 ili kutinga fainali za Ulaya baada ya misimu kadhaa ya ukame wa taji hilo tangu ilipotwa mara ya mwisho mwaka 2002.
Hata hivyo huenda isiwe kazi rahisi kwa vijana wa Santiago Bernabeu kutokana na ukweli wapinzani wao wapo vyema msimu huu licha ya kutemeshwa taji la ubingwa wa Bundesliga na Bayern Munich.
Dortmund wanasaka heshima baada ya kutwaa taji hilo mara ya mwisho mwaka 1997, hivyo huenda hawatakubali kuipoteza nafasi waliyopata safari hii kwa mabao manne ya Robert Lewandowski aliyefunga katika pambano la awali wiki iliyopita.
Wakati hatma ya Madrid na Dortmund ikitarajiwa kufahamika usiku wa leo, mabingwa wengine wa zamani wa Ulaya, Barcelona na Bayern Munich zenyewe zitakuwa na kibarua kingine kesho nchini Hispania.
Barcelona iliyocheze kichapo cha aibu wiki iliyopita ugenini kwa kulala kwa mabao 4-0 itakuwa nyumbani kujaribu kutupa karata yake kwa wageni wao ambao msimu huu wanatisha kisoka barani Ulaya.
Ikiwategemea nyota wake kama Xavi, Iniesta, Cesc Fabregas na Lionel Messi, Barca itakuwa na kazi pevu kulipiza kisasi na kutaka kupenya katika pambano hilo ili kucheza fainali Mei 25 itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley, Uingereza.
Je, ni Wahispania au Wajerumani watakaoenda London kwenye fainali hizo? Tusubiri tuone maana soka lina maajabu yake.

Kesho ni siku ya Wafanyakazi Duniani, Kero za wafanyakazi zitafutiwe ufumbuzi


Kwa miaka mingi sasa wafanyakazi wa umma na hata wa sekta binafsi wamekuwa wakilalamikia kiwango kidogo cha mshahara wanacholipwa kwamba hakiendani na hali ngumu ya maisha inayowakabili.
Kwa maana rahisi ni kwamba mishahara wanayolipwa wafanyakazi nchini haiwezi kumudu gharama za maisha kwa mwezi, hivyo wengi wanaishi katika maisha ya dhiki na kubahatisha.
Kibaya zaidi, tatizo hili la nyongeza ya mshahara kutoendana na hali halisi ya maisha linaathiri zaidi wafanyakazi wa ngazi ya chini ambao ndio wengi hivyo kuwapotezea ari ya kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya nchi yetu.
Hivyo basi, wakati tunajiandaa kusherehekea Siku ya Wanyakazi Duniani kesho, ni vyema mgeni rasmi wa maadhimisho hayo nchini ambaye ni Rais Jakaya Kikwete ajibu kero mbalimbali zinazowakumba watumishi hawa ambao waliitikia wito wa kuitumikia nchi kwa uaminifu.
Tunatambua kwamba Serikali haiwezi kuwa na uwezo mkubwa wa kumaliza tatizo la viwango vidogo vya mshahara kwa mara moja, lakini tuna imani kwamba kwa kiasi fulani inao uwezo wa kupunguza tatizo hili kwa zaidi ya nusu hivyo kutoa matumaini mapya kwa wananchi.
Sote tunambua kwamba katika miaka ya hivi karibuni mfumuko wa bei umepanda kwa kasi ya ajabu hivyo kufanya bidhaa kuuzwa kwa bei ghali. Kupanda huku kwa mfumuko wa bei, kumefanya watu wengi wakiwamo wafanyakazi kushindwa kununua baadhi ya bidhaa ambazo hapo awali walikuwa wakizinunua kwa mahitaji yao ya kila siku.
Ndiyo maana tunasema kwamba kima cha chini cha mshahara ambacho ni Sh180,000 hakilengi kumsaidia mfanyakazi kuishi maisha ya kawaida ya binadamu bali kinamfanya aendelee kudhalilika kwa dhiki isiyo na kifani.
Lakini pia wakati tukiiasa Serikali kupandisha kima cha chini cha mshahara, upande wa sekta binafsi nako hali ni mbaya sana, kwani mishahara ni midogo na tunaambiwa kwamba kuna waajiri wengine hasa wa sekta ya ulinzi wanawalipa watumishi wao kiasi cha Sh40,000 hadi Tsh 60,000 kwa mwezi.
Kweli hii si haki, hivyo hatua kali lazima zichukuliwe dhidi ya unyama wa aina hii. Sote tunajua kwamba Serikali imeweka viwango vya mshahara katika sekta binafsi hivyo ni kosa kwa waajiri hawa kutofuata miongozo halali.
Mbali na mishahara, madai mengine ambayo wafanyakazi nchini wamekuwa wakilalamika kila mwaka ni kodi kubwa inayotozwa kwenye mishahara. Hivyo basi tunaona ni wakati mwafaka kwa tatizo hili kufanyiwa kazi, ikiwa ni pamoja na Serikali kutafuta maeneo mengine ya kukusanya kodi badala ya kutegemea kwenye mishahara midogo ya watu wa chini.
Ndiyo maana kama taifa ni lazima sasa tukae chini na kumaliza tatizo la mishahara nchini.
Kwa bahati nzuri, katika hotuba yake kwenye kilele cha sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Rais Kikwete alisema Serikali inatambua mazingira magumu ya kazi waliyonayo wafanyakazi na kwamba Serikali ipo tayari kuyaboresha.
Kutokana na kauli hiyo ya Rais Kikwete, bado tunaamini kwamba Serikali yake ina dhamira ya dhati ya kusaidia wafanyakazi nchini nao waishi kama wengine wanaofaidi rasilimali za nchi yetu.
Tunaamini kwamba kilio cha wafanyakazi kikisikilizwa na migongano ya hapa na pale na Serikali itakuwa historia kwa lengo la kusukuma mbele maendeleo yetu.
Vilevile, tunatambua juhudi mbalimbali za Serikali za kukabiliana na tatizo la mfumuko wa bei na kwamba ziendelee kwani zitasaidia wafanyakazi waishi katika mazingira bora ya kuwafanya wajitume ipasavyo.
Mwananchi

Saturday, April 27, 2013

Mnyika amshitaki Ndugai kwa wapiga kura wake

Mbunge wa Jimbo la Ubungo wa Chama cha Demokrasia 
na Maendeleo (Chadema), John Mnyika.
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo na Kiongozi wa Kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amemshitaki Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai kwa wapiga kura wake, akiwahoji iwapo walimtuma bungeni kufanya Ubabe wa kuwatoa nje wabunge wenzie badala ya kuwatetea.
Mnyika alitoa Mashitaka hayo jana Aprilli 26, 2013 katika kijiji cha Iyegu, Kata ya Mlali, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, ambapo alisema amemkatia Rufaa Ndugai mara Tano bungeni bila majibu, kwa hiyo jana aliamua kumshitaki kwao ili wafanye maamuzi magumu juu ya mbunge wao asiyefanya kazi waliyomtuma.
Akizungumza katika Mkutano huo Mnyika alimshitaki Ndugai akiwahoji kama walimtuma kufanya hivyo, na waliposema Laa, aliwataka kufanya mabadiliko ya mwakilishi wa Jimbo lao kama wanataka kumaliziwa Kero zao zikiwepo Haki na Maendeleo ya kiuchumi na Matumizi bora ya Rasilimali zao.
Mwananchi mmoja alimhoji Mnyika “Je, ni nani aliyetayarisha, kulinda, kusimamia na kusafirisha Twiga wetu kwenda nje, lini watarejeshwa na waliohusika watafanywaje?.
Mnyika aliwajibu wananchi kwamba, wahusika wa usafirishaji wa Twiga wao ni vigogo walioko madarakani, na Twiga hao wako nchi mmoja ya Kiarabu, na mbali ya Twiga hao hivi karibuni Chadema itaibua suala la Tembo, na kuwaambia suluhisho la haraka kwa yote hayo ni kufanya mabadiliko ya viongozi mafisadi haraka.

Alipoulizwa Mauaji na Vitisho wanavyofanyiwa na Kundi linalojiita Kanyaga Twende, wanapoamua kujiunga na vyama Upinzani, Mnyika aliwauliza kama wanayo simu ya Mbunge wao wamuulize ila wasimtukane, na waliposema hawana aliwatajia namba ya Ndugai na ya Mkurugenzi wa Usalama Chadema ambaye alidai atawawasaidia dhidi ya vitisho .
Aidha Mnyika kabla ya kushuka Jukwani saa 11.30 jioni, aliuuliza umati uliokuwepo uwanjani hapo, wangapi wapo tayari kwa mabadiliko ya M4C, watu wote karibu 1,000 walinyosha mikono na Mnyika akashuka kuelekea Kongwa kuungana na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, kuendelea na Mikutano mingine.

HAYA NDIYO MAKOSA MATATU YALIYOMNYIMA DHAMANA MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA JANA JIONI NA KUSUBIRI KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU

Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jana  jioni ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui
i)Kosa la kwanza ni..
kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’Huu nao umeitwa kwamba ni uchochezi.

Maneno ya hapo juu ndiyo yaliyosababisha jeshi la polisi kuvamia nyumbani kwake usiku wa manane ....

Huo umeitwa uchochezi baada ya mkuu wa mkoa kumtumia ujumbe wa mkononi kupitia simu yake kupitia namba 075296027*  aliyotishia kumbambikizia kesi anayoitaka yeye

Friday, April 26, 2013

AIBU: BI HARUSI AKAMATWA AKIFANYA NGONO KWENYE BAJAJI,MTOTO WA KIGOGO NAYE NDANI.

clip_image002[4]
NI aibu sana! Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Oparesheni ya Fichua Maovu iliyosimamiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar, OCD Wilbroad Mutafungwa na Ofisa wa Oparesheni, Inspekta Jacob Swai kwa kushirikiana na Global Publishers iliyonasa wanawake wanaojishughulisha na mambo ya ngono usiku kucha.Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo (jina linahifadhiwa).
BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ
Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.

Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

clip_image002[6]BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.

 
MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE
clip_image002Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.

MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.

ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?
Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.
INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.
NI MATOKEO YA GAZETI LA RISASI
Oparesheni hiyo ilikuja siku chache baada ya gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 1000 la Jumatano ya Aprili 17-19 kuripoti ufuska unaofanyika katika ufukwe huo usiku wa saa 9 na kuendelea. 
Uchunguzi wa gazeti hilo ulieleza kiundani vitendo vya ngono, usagaji, ubakaji, ushoga na ujambazi vilivyokuwa vikifanyika eneo hilo hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni wakaona kuna kila sababu ya kufumua uozo huo kwa kuwa ni wachapakazi.

Source: GP

BREAKING NEWS ZA MSIBA!open link yawezekana ukasaidia.

Msiba New Jersey

Kuna kijana amefariki New Jersey, USA. Kijana aliyefariki alinajulikana kwa jina la Adolf, Brian au Tadeous Rwekagende. Alikua anasema alisoma Tambaza na alikua na mdogo wake anaitwa Rodrick Rwekagende ambaye naye alikua anaishi Texas. Ila cha kusikitisha ni kuwa huyo mdogo wake alisema alifariki mwaka jana mwezi wa nne (Tanzania).

Adolf alikua anasema baba yake na mama yake walifariki yeye na mdogo wake huyo wakiwa wadogo. Sasa yeye alikulia kwa mjomba wake. Juzi Adolf alipata massive stroke na kulazwa st Barnabas hospital, Livingston, NJ na kufariki. Mpaka sasa hivi kuna watu wametafuta ndugu zake na kumpata mjomba wake mmoja huko Bukoba vijijini. Hatukuweza kupata ndugu wa karibu hapa marekani na mpaka sasa hivi maiti yake ipo hospital haijawa claimed. Hivyo kama binadamu tumeamua kujichangisha ili tuweze kupeleka mwili wa mwezetu Tanzania kwa mazishi. Gharama za kuzika huku na kusafirisha kupeleka Tanzania ni karibu sawasawa tu hivyo tunaona ni bora akapumzike na ndugu zake Tanzania.

Hivyo tunaomba mtupostie kwenye blog zenu hili tangazo liwafikie watanzania watakaopenda kumsaidia ili apelekwe Tanzania tutashukuru sana. Tumefungua mahali pa kuchangisha hela http://www.donationto.com/adolfsendhomecost  au kama mtu anatumia paypal account ni adolffuneralcost@gmail.com. Tutawapa majina ya watu watakaokua kwenye kamati ya kukusanya hela mara tutakapomaliza kikao tunachotegemea kufanyika Jumamosi. na hela zote zitaonyeshwa zilivyotumika kama zipo extra zitapelekwa huko kwa wajomba zake Bukoba.

Na kama kuna mtu ana picha yake basi mtutumie kwa sababu hakuna mtu aliye na picha yake. ID yake ipo hospital hawawezi kumpa mtu mpaka wakishajua nani anachukua mwili na mahali alipokua anaishi hawaruhusu mtu kuingia kwa sasa mpaka wakishajua mazishi ni wapi au ndugu wa karibu ni wapi. Hivyo hamna mtu ana picha yake..

Please sisi hapa tunajitahidi ili azikwe kama ubinadamu hivyo huu sio muda wa kuanza kuuliza maswali kwa nini hiki wala kile...Kwa vile hata sisi tuna maswali mengi na hakuna mtu mweye

jibu....Tunachojua ni kuwa alipata massive stroke na amefariki na hakuna ndugu  yake wa karibu huku marekani.

Tunatanguliza shukurani na pia kama blog yako hupost mambo ya habari tunaomba utusaidie kuforward hii email kwa watu wengine...Kuna wazee wako NY kama wakikukubali kushughulikia huu msiba tutawatangazia na kuwapa information mpya.  Na hela zitakazopatikana zitahamishiwa kwenye fund yeyote watakayofungua kama wataamua kufungua mpya au wataamua kuendelea na hi hii.  Tunachotaka ni kusafirisha kijana wa watu Tanzania kwa sababu sasa hivi hilo ndio lengo letu....na hakuna mtu yeyote aliyesema kitu chochote hivyo kama kikao kikifanyika basi tutawaeleza linaloendelea.

Nitajitahidi kuupdate kinachoendelea katika twitter handle yangu @swahilimom
Regards,
Pauline

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA MUUNGANO UWANJA WA UHURU LEO

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiingia uwanjani katika gari maalum huku akisindikizwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange. 

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo kuongoza Watanzania kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Pamoja naye kwenye gari hilo la wazi ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange
 Nyomi si ya kawaida hata pa kutema mate hakuna
 Msafara wa Rais Kikwete ukizunguka uwanja wa Uhuru
Nyomi ya leo. Taswira zingine na kumwaga baadaye.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama lililoandaliwa maalum kwa ajili maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kwenye uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na Mabalozi pamoja na wageni waalikwa mbalimbali ili kushuhudia maadhimisho hayo.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akikagua kikosi cha Jeshi la Magereza wanawake wakati wa maadhimisho hayo Rais Dk. Jakaya Kikwete akielekea jukwaani mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama katika maadhimisho hayo Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine kutoka kulia ni Rais Mstaafu Benjamin Wiliam Mkapa, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Kutoka kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kulia akiwa na viongozi wengine katika jukwaa kuu kutoka kushoto ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Idd, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo. Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Uhuru Msafara wa Rais ukiingia uwanjani leo Kikosi cha Jeshi la Ulinzi JWTZ kikipita na kutoa heshima mbele . Kikosi cha Jeshi la Ulinzi JWTZ wanamaji kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete . Kikosi cha Jeshi la Kujenga taifa JKT kikitoa heshima mbelea ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete. Kikosi Maalum Cha Bendera kikitoa heshima zake bele ya Rais Jakaya Kikwete Kikosi chamJeshi la Ulinzi JWTZ nchi kavu kikipita na kutoa heshima mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete. Kikso cha Askari wa Magereza kikipita na kutoa heshima mbele ya Rais Jakaya Kikwete Watoto wa halaiki wakionyesha ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano wetu mbele ya Rais Jakaya Kikwete na maelfu ya Watanzania waliohudhuria katika maadhimisho hayo Watoto wa halaiki wakionyesha ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano wetu mbele ya Rais Jakaya Kikwete na maelfu ya Watanzania waliohudhuria katika maadhimisho hayo.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-UWANJA WA UHURU)

MATUKIO YOTE MAANDALIZI YA MAZISHI YA MWANAFUNZI ALIYE UWAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MWILI WAKE UKIWASILI IRINGA LEO HII TOKA ARUSHA


MWILI  WA MAREHEMU  UKIINGIZWA  KANISANI TAYARI KWA KUSALIWA

NJE YA KANISA

DIAMOND AWATAKA MADEMU WA LONDON WAJIPENDEKEZE ILI ACHAGUE WA "KUMKANYAGA"


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaendelea kutunisha akaunti yake baada ya kulamba shavu la shoo za kutosha nchini Uingereza ambapo ameahidi kurejea Bongo na mchumba rasmi atakayemtambulisha kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’.
  
Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo juzikati kupitia website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba’ke.

Bila kujali mjadala utakaoibuka kwa kuwa tayari ana mchumba ambaye ni Penniel Mungilwa ‘Penny’, Diamond alifunguka: “Mashabiki wangu wa London na Reading kijana wenu nakuja kuweka historia kwa mara nyingine. Warembo mpendeze nakuja kuchagua mchumba mmoja wa kuja kumtambulisha kwa mama Diamond.”

ZITTO KABWE ATOA POLE KWA FAMILIA YA GODBLESS LEMA BAADA YA KUTIWA MABOMU JANA USIKU

 Hii  ni  kauli  ya  Zitto  kabwe  Baada  ya mbunge  wa  Arusha  kutiwa  mbaroni  jana  usiku..

BREAKING NEWS: Mbunge wa Arusha Mjini kupitia chama cha Demokrasia ma Maendeleo (CHADEMA) Ndugu "Godbless Lema" usiku wa jana kuamkia leo saa8 amefikishwa Central Police bila kufahamika chanzo...
 Hii inatupa wasiwasi na kubaini kua kuna mchezo nyuma ya pazia unaochezwa na kundi la watu wa chache katika siasa upande wa pili wa upinzani kibaya zaidi ni ma'askari waliovamilia nyumbani kwa mbunge usiku wa jana na kulipua mabomu na wakiwa na silaha kali utadhani wamekwenda kumkamata jambazi au mtu mwenye kesi ya mauaji kitu ambacho sio kizuri. 
#Pole kwa familia ya Godbless Lema.

PROFESA LIPUMBA AIPONDA CHADEMA NA KUDAI KUWA NI VINARA WA VURUGU NA HAWANA HOJA


Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema vurugu zinazoendelea bungeni zinasababishwa na Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kushindwa kujenga hoja na mbinu za kuwabana wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wabunge wa Chadema wana tabia ya kufuata mfumo wa kwenda bungeni na hoja zinazobeba chama chao na si za Watanzania wote kama jinsi CCM wanavyofanya.


“Kambi rasmi ya upinzani imepoteza uwezo wa kujenga hoja za mashiko na mbinu madhubuti za kuwabana wabunge wa CCM bungeni na badala yake Chadema, wamekuwa na tabia mbaya ya kubeba chama chao,” alisema Profesa Lipumba.



Alisema kambi rasmi ya upinzani pia imeshindwa kulinda utaratibu mzuri wa kutetea masilahi ya umma bila jazba na hoja zenye mashiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ilipokuwa ikiongozwa na CUF, Kiongozi huyo alisema kambi ya upinzani inapaswa ijipange upya kwa utaratibu na mikakati mizuri ya kuteta hoja za wananchi bila kuyumbishwa na wabunge wa CCM.


“Bunge usiwe uwanja wa kuonyesha mbwembwe za chama bali uwe uwanja wa kutetea haki za wananchi, wabunge wanapaswa wabadilishe mitazamo ya kuona bungeni ni sehemu ya kujionyesha kisiasa na chama chako kinafanya nini nje ya Bunge,” alisema Lipumba.



Alisema viongozi wa Serikali wanapaswa kubadilika kuhusu namna ya kutoa majibu bungeni.


Profesa Lipumba alisema mawaziri wengi wanakuwa wakitoa majibu mepesi katika maswali ya msingi yanayoulizwa na wabunge wa upinzani.


Alisema Bunge linatumia muda na pesa za walipakodi vibaya kwa baadhi ya wabunge kuwa na ubishi usiokuwa na tija, kutoleana matusi na wengine kuingilia hoja za wenzao bila sababu za msingi.


Profesa Lipumba pia alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda amepoteza uwezo wa kuliongoza Bunge.


Mwananchi

ARSENAL YAZINDUA RASMI JEZI MPYA MSIMU UJAO

image

Afrika Mashariki:Tanzania tajiri wa madini, Gesi watu maskini

Nchi ya Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na watu maskini kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ikiongozwa na Burundi.
Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) mwaka huu, umebaini kwamba katika nchi za Afrika Mashariki, Uganda inaongoza kwa kutokuwa na watu maskini.
Utafiti huo ulibaini Tanzania ina asilimia 67.87 ikifuatiwa na Burundi ambao wana asilimia 81.32. Ukiacha Tanzania nchi inayofuatia ni  Rwanda ambayo utafiti huo ulibaini kuwa ilikuwa na asilimia  63.17, huku  watu wa Kenya wakiwa na alama za umaskini kwa asilimia 43.37,  Uganda 38.01.
Kwa mujibu wa ripoti ya Global Monitoring ya mwaka 2013, matokeo ya utafiti huo yaliangalia idadi ya watu wanaoishi kwa Dola 1.25 sawa na Sh2,000 kwa siku.
Kwa utafiti huu, Tanzania na Burundi zinakuwa nchi zenye idadi kubwa ya watu maskini katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi za chini ya jangwa la Sahara zinajikongoja katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia. Mwaka 1990 nchi za chini ya Jangwa la Sahara na Asia Mashariki zote zilikuwa na asilimia 55 wakati zilipoanza safari ya kuelekea maendeleo ya milenia.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo,  mwaka 2010 Asia Mashariki ilifanya jitihada kubwa za kupunguza umaskini hadi kufikia asilimia 12 wakati nchi za chini ya Jangwa la Sahara zilikuwa zina asilimia 48 ya umaskini.
Barani Afrika ukuaji wa miji umeongeza kutoka asilimia 30 mwaka 1980 hadi asilimia 50 mwaka 2011.
“Ukuaji wa miji unasaidia watu kuondokana na umasikini na kuelekea katika malengo ya Milenia, lakini kama hautasimamiwa vizuri unaweza kusababisha ukuaji holela wa miji, uchafuzi wa mazingira na ongezeko la uhalifu,” inasema ripoti hiyo.
Zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa zinazozalishwa ulimwenguni zinazalishwa mijini, na kusababisha ukuaji wa miji na kupunguza umaskini. Nchi nyingi za Asia Mashariki na Marekani zimefanikiwa sana kupunguza umaskini kwa kupiti njia hii.
“Kinyume chake, Asia Kusini na nchi za chini ya Jangwa la Sahara zina idadi kubwa ya watu maskini na zinaendelea kujikongoja kuelekea katika maendeleo ya Milenia.” inabainisha sehemu ya ripoti hiyo ya WB.
Wachumi Tanzania
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tanzania, Dk Honest Ngowi anasema kimsingi umaskini ulioanishwa na ripoti hiyo ni umaskini wa kipato na anasema licha ya kuwa tuna raslimali nyingi kama madini, utalii na nyingine, lakini hoja inayokuja ni je zinatumiwa vipi?
“Ni sawa madini yanachimbwa, lakini wawekezaji ndiyo wengi, lakini sekta hii ya madini haina mwingiliano wa moja kwa moja na watu, na kama watu wa kawaida hawahusiki moja kwa moja inakuwa vigumu kuinuka kimapato,” anasema mhadhiri huyo.
Mtaalamu huyo wa uchumi anabainisha kwamba ili mtu awe na kipato ni lazima afanye kazi.
“Kama watu wengi hawafanyi kazi ni lazima umaskini utaendelea,” anasema.
Dk Ngowi anasema hapana budi kuwashirikisha wananchi katika soko la ajira na  masuala ya ujuzi yanachukua sehemu kubwa. Dk Ngowi anakiri kuwa mambo hayo ni changamoto kubwa kwa Taifa.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Profesa Humphrey Moshi anasema uchumi wa Tanzania ambao umeripotiwa kukua katika kipindi cha miaka 10 haupunguzi umaskini.
“Uchumi umekuwa ukiwanufaisha watu wachache, zaidi umekuwa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Arusha,” anasema Prof. Moshi.
Profesa huyo anasema kuwa inabidi sera za uchumi zibadilishwe kwa kupunguza pengo la kiuchumi lililopo kati ya maeneo ya mijini na vijijini.
Anasema kuna hali kubwa ya matabaka  na watu  walionacho wanazidi kupata huku maskini wakizidi kuwa maskini.
Mhadhiri huyo wa UDSM anasisitiza zaidi kwamba sekta ya viwanda haina budi kuboreshwa kwa kuhakikisha kuwa inakua.
Kuhusu kilimo, Profesa Moshi anasema licha ya kuwa sekta hiyo inaajiri watu wengi, lakini haipati raslimali za kutosha.
Watanzania wanazidiwa na wenzao wa EAC licha ya nchi hii kusifika kwa kuwa na rasilimali nyingi kuliko majirani hao.
Tanzania ina ardhi kubwa inayofaa kwa kilimo na  wataalamu kadhaa wamewahi kueleza kuwa Mkoa wa Morogoro peke yake ukitumiwa vyema unaweza kuzalisha chakula na kukidhi mahitaji ya nchi nzima.
Madini kama Tanzanite ambayo yanapatikana Tanzania peke yake bado hayajawanufaisha Watanzania na inasemekana yamekuwa yakiuzwa nchi jirani badala ya soko lake kuwa nchini.
Dhahabu na almasi ni madini mengine ambayo kama yangetumiwa vyema Tanzania isingetupwa mbali na wenzake. Pia gesi ni gezo kingine cha kuwaondoa watu kwenye umaskini.
Mbali na hayo Taifa lina raslimali nyingine kama vivutio vya kitalii na mapema mwaka huu vivutio vyake vitatu Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Ngorongoro na Serengeti  vilishinda katika maajabu saba ya asili barani Afrika.
Katika nchi hizo tano za EAC Tanzania ndiyo yenye eneo kubwa yenye kilometa za mraba 945.0870, na pia ina idadi kubwa ya watu 44.9 milioni ambao ni raslimali kubwa zaidi ya uzalishaji na ukuzaji wa uchumi. Kenya ina watu 38.6 milioni kwa mujibu wa sensa ya 2009, na Uganda watu 32.9 milioni.
Hali inazidi kuwa ngumu zaidi kwa sababu gharama za maisha zinapanda kila siku.
Mkazi wa Tabata Kisukuru jijini Dar es Salaam, Magreth Lucas ambaye anafanya kazi ya Mamalishe anasema hali ni mbaya  kwa sababu gharama za maisha zimepanda.
“Kila kitu kimepanda, nauli juu, sokoni vitu bei juu hata biashara imekuwa ngumu wateja nao wamepungua,” anasema mama lishe huyo anayefanya biasharakatika  eneo la Tabata Relini.
Magreth anasema fedha anazopata anashindwa hata kuweka akiba kutokana na ugumu wa maisha na anafafanua kwamba analipa kodi ya nyumba Sh30,000 kwa mwezi,  nauli ya kila  siku Sh400 na chakula kila siku Sh2,000, hakuna kinachobaki
Mwananchi

MZIMU WA MICHAEL JACKSON WAWASUMBUA NDUNGU ZAKE....

MICHAEL Jackson’s sister La Toya has claimed the late singer is haunting his childhood home.

The 56-year-old believes Jacko’s spirit is looking over his children Prince, Paris and Blanket — who live there with his mum Katherine.

And she said the superstar can be heard tap dancing in the mansion in Encino, California.

The former Celebrity Big Brother star said: “You don’t see anything but you feel a presence.”

La Toya has also been using a psychic to speak to her brother, who died of an overdose in 2009 aged 50. She said: “If Michael wants to tell me something, I want to know.”
Source: thesun.co.uk

DIAMOND PLATINUMZ KUWASHA MOTO LONDON KESHO

BAADA YA ZITTO, NASSARI NAYE AANDIKA UJUMBE KUHUSU KUKAMATWA KWA LEMA USIKU WA JANA


Posted in , ,
 
Nimepata kwa mshtuko na nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha wamevamia na kuizingira nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.
Nimelazimika kumpigia simu RPC kuthibitisha na cha ajabu akaniambia ni kweli.
Nimemshauri kama kiongozi mwenzake mwenye dhamana ya kusaidia kuilinda
kweli na haki ili kuleta Amani ya kweli kwenye mkoa wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema achilia mbali Kiongozi mkubwa kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi usa river au unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni mkiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya uvunjifu wa amani, kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.
Nyumbani kwa mbunge hakai mbunge mwenyewe. Kuna watoto akiwemo mwenye umri wa miezi mitano, mke, ndugu etc. Utapigaje mabomu kwenye nyumba hii, bila shaka yatakuwa mauaji. Lema si jambazi, ni kiongozi, ni role model, ni raia mwema sana na mzalendo kwa taifa lake.
Hii wapi sababu ya kuvamia kwake usiku na kuwapa wanafamilia pychological tortue.
Kama amenielewa atasikia, otherwise "truth will always stand" . Tuko tayari na tulishakuwa tayari, hatujashtukizwa. Tunaendelea kuongezewa kura za madiwani arusha juni 16, 2013. Ni vyema watawala wakakumbuka habari ya Farao na Mungu juu ya mateso ya wana wa Israel utumwani. "Mungu akaufanya moyo wa farao kuwa mgumu, ili azidi kujidhihirisha kwa wana wa Israel"

Thursday, April 25, 2013

PICHA ZA MWIGIZAJI KUTOKA NIGERIA ALIYELIPWA N5,000,000 ILI ANYOE NYWELE, AKINYOLEWA KWA WEMBE

chika ike goes bald 5 million
chika ike shaves hair for 5 million
chika ike cuts hair
Nigerian actress Chika Ike alias Fancy Nancy has sacrificed beauty for money.

The talented actress cuts her hair on Monday the 22nd of April for a whopping N5 million reward.

Chika Ike is following the footsteps of other Nollywood movie stars like Mercy Johnson, Oge Okoye and many others who shaved their own hairs for a rewarding movie role.

In moments of tears Nigerian movie, the actress played the role of the youngest wife of veteran actor Olu Jacobs… when he eventually dies, she shaved her hair to mourn him.

The actress is not without controversy. Critics are currently blasting her for showing off her N5 million cheque since others who shaved their hair before her didn’t do such.

TOTO AFRIKA, AFRIKA LYON ZAAGA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA, ZASHUKA RASMI.


Kwa ufupi
Timu moja kati ya tatu, yaani Polisi Moro, Mgambo na JKT itashuka daraja ili kuungana na Toto na Lyon kukamilisha timu tatu zitakazokwenda daraja la kwanza msimu ujao.
 Timu ya Toto African Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, akichuana kuwania mpira na Emmanuel Swita wa Toto Afrika wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodocom Tanzania bara. KIKOSI CHA AFRICAN LYON.Mshambulia wa Polisi Morogoro Nohoda Bakari akiwania dhidi ya mlinzi wa African Lyon ya Jijini Dar es Salaam, Hood Mayanja kulia wakati wa mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo katika mchezo huo African Lyon ilikubali kipigo cha bao 1-0 na kuendelea kuburuza mkia katika mzunguko huu wa pili wa ligi hiyo. 

DAR ES SALAAM. 

TOTO African ya Mwanza na African Lyon ya Dar es Salaam, jana zimekata rasmi tiketi ya kurudi daraja la kwanza msimu ujao kufuatia kuathiriwa na ushindi wa bao 1-0 waliopata JKT Ruvu dhidi ya Lyon katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa jana.

Kwa ushindi huo, JKT Ruvu imefikisha pointi 26 ambazo haziwezi kufikiwa na Toto African yenye pointi 22 hata kama itashinda mchezo wake mmoja uliobaki.

Lyon iliyohitaji kushinda mechi ya jana ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kubaki Ligi Kuu, ina pointi 19 na hata kama itashinda mechi mbili zilizobaki itaishia pointi 25, ambazo tayari zimeshapitwa na JTK.

Timu moja kati ya tatu, yaani Polisi Moro, Mgambo na JKT itashuka daraja ili kuungana na Toto na Lyon kukamilisha timu tatu zitakazokwenda daraja la kwanza msimu ujao.


Ili kujinusuru, Mgambo yenye pointi 25, Polisi pointi 19 (michezo mitatu mkononi) na JKT pointi 26, zitalazimika kushinda mechi zao lakini pia zikiomba ‘wahanga’ wenzao wapate matokeo mabaya.

Katika mchezo wa jana kwenye Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Mussa Mgosi alikaribia kufunga bao dakika ya sita kama siyo shuti lake kali kupaa juu kidogo ya lango la African Lyon, kama alivyofanya mshambuliaji wa Lyon, Adam Kingwande.

Emmanuel Pius alibadilisha matokeo kwa kufunga bao la kwanza kwa Ruvu katika dakika ya 18 akimalizia pasi ndefu ya Ramadhan Madenge, huku Lyon wakishindwa kusawazisha dakika ya 31 na 50 kupitia kwa Kingwande.

Lyon waliendelea kusaka bao la kusawazisha na nafasi nzuri ilipotea dakika ya 55 baada mpira wa kona uliochongwa na Mohamed Samatta kwenda kugonga ‘paa’ kutoka nje.


Simba inaingia uwanjani leo kucheza na Ruvu Shooting katika mchezo wenye sura zaidi ya kulinda heshima, kwani tayari imeshautema ubingwa na hakuna uwezekano wa kushika nafasi ya pili.

Kwa sasa mabingwa hao wa msimu uliopita, wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 36, kama ilivyo kwa Mtibwa inayoshika nafasi ya tano.

Kama timu ya Simba watashinda mechi zote zilizobaki watafikisha pointi 48, Timu ya Kagera Sugar inayoshika nafasi ya tatu itakuwa na pointi 49 na Azam katika nafasi ya pili watafikisha pointi 52.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo Jamhuri Kihwelu, alisema jana kuwa wapo katika harakati za kupigania nafasi hiyo na wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanashinda mechi zote zilizobaki ili kulinda heshima.