Najua kwa jinsi hali ilivyo itakuwa vigumu kunijibu. Ila napenda ifahamike tu kuwa binafsi majibu siyahitaji sana ila nikiona utekelezaji wa haya nitafarijika sana. La ikiwezekana kujibu pia nifurahi.
Kuna
wakati niliwahi kuandika (kwa katibu mkuu) kuhusu wasiwasi wangu
kutokana na tabia za kinafiki za Serikali pamoja na chama kinachounda
serikali. Nilikita hofu yangu zaidi kuhusu uliokuwa mtazamo wa wazi wa
serikali wa kutotambua wala kuona umuhimu wa Katiba mpya nchini. Sikuwa
nimeridhika na kitendo cha serikali kuamua ghafla kushika kibendera cha
katiba wakati Waziri mwenye dhamana akishirikiana na mwansheria mkuu
walitoa tamko kwa niaba ya serikali yao kuwa Tanzani haiko tayari na
hakuna haja. Nilieleza wasiwasi wangu kuwa ile ni njia ya kunyamazisha
mabadiliko ya kweli kwa serikali kutafuta uhalali wa kujipa nafasi ya
kuendesha mabadiliko yatakayopelekea kupatikana kwa katiba isiyo ya
wananchi na kwa maslahi ya CCM. Nlisisitiza kuwa Haiwezekani kupata
katiba nzuri kama mchakato wa kupata katiba una kasoro tayari. Nilisema
kuhusu upatikanaji wa waumbe wa mabaraza ya katiba (yote),kuwa sheria
iliyopitishwa haikidhi kwa kushindwa kufafanua namna wawakilishi wa
makundi maalum watakavyopatikana. Kuna kipindi niliwahi kuandika kwenye
mtandao wa kijamii (jamii forrums-reffer to Elly BM posts) kuwa hali
hiyo inakoenda itapelekea vyama vya upinzani na wanaharakati kuamka
mwishoni kwa kuona kuwa mchakato una kasoro nyingi, hivyo kugomea
mchakato, hivyo kupelekea aidha kupatikana katiba isiyo na ridhaa ya
wanachi(ambayo nilitabiri itakuwa mbovu kuliko iliyopo) au kutokuwa na
katiba mpya. Nilimalizia kuwa kwa ninavyoona yote hayo yana lengo la
kuifanya CCM irudi madarakani 2015! Inanisikitisha kuona kuwa hayo yote
ndiyo yanayotokea kwa sasa.Nahofia zaidi kuwa lile nililoona linakuja
huenda likatokea.
Kwa muda
mrefu kumekuwa na tatizo kubwa la serikali kutumia udhaifu wa wananchi
kukwepa kutoa majibu stahiki kwa matatizo ya wananchi. Mpaka sasa nna
uhakika kuwa serikali ilishaona kuwa watanzania wana desturi ya kuja na
hoja kwa nguvu sana lakini baada ya muda, au baada ya kuzuka jambo jipya
wanasahau na kuacha ya jana. Nadhani wote tutakumbuka jinsi hoja za
upungufu wa umeme zilizotakiwa kutolewa majibu na serikali na TANESCO,
lakini ikaishia kuzusha tiba ya BABU wa Loliondo. Media yote ikaacha
Umeme ikabaki Loliondo. Mpaka leo umeme siyo wa uhakika, kina January
makamba ni mawaziri wadogo na umeme hakuna anayesema waziwazi ni nini
kimetokea! Waziri Muhongo anatangaza uharamu wa nguzo za South Africa na
ubora wa nguzo zetu, sikuchache baadaye anasema za kwetu siyo bora,
tutaendelea kuagiza kutoka nje, na bado anaendelea kuwa Waziri, anakuja
Bungeni na anaangaliwa!
Mpaka sasa
bado wanachi wanapenda kujua ni kwa nini serikali ilisababisha mauaji
ya raia wasio na hatia Arusha, na kwa nini Waziri mkuu alidanganya Bunge
na wanachi na mpaka sasa hakuna majibu yaliyotolewa. Bado wananchi
hawajui hatima ya madeni ya Dowans na kama hayalipwi. Bado hoja za
Meremeta na EPA hazijashughulikiwa ipasavyo, wala haijulikani kama kama
ni lini kutatolewa maibu ya msingi. Mifano ya aina hii ni mingi.
Leo
naomba nielezee hofu yangu juu ya hali hiyo. Kwa ninavyoona
imeshazoeleka kuwa vyama pinzani vinatoa hoja za msingi, serikali na CCM
vinajibu juujuu, majibu ya kitoto na yasiyoridhisha kabisa. Megine
mpaka leo yanasubiri kutolewa miongozo na Spika wa Bunge mwenye ridha za
CCM, ambaye mpaka sasa ameshindwa kabisa, yeye na Naibu wake kuonyesha
walau ukomavu kidogo na kuepuka japo kinafiki tu ile hali ya wazi
inayoonekana kuwa anafanya kazi za chama chake Bungeni na anadhibiti
wabunge wa upinzani kwa kupindisha kanuni za bunge. Mpaka sasa majibu ya
msingi kwa hoja zote za upinzani ni kuwa Wapinzani ni wazushi na
wachochezi, wenye lengo la kutaka nchi isitawalike tu. Na ni mbaya sana
kwani inapofikia hapo hiyo ndiyo inakuwa hoja ya mwisho inaachwa hivyo.
Naogopa kuwa siyo wananchi wote wana uelewa wa kutosha, hasa vijijini,
kuhusu siasa za Tanzania. Nafikiri inaweza kufikia wananchi wa kawaida
wakakubaliana na propaganda kuliko ukweli. na hili wote tunajua athari
yake kwa mabadiliko ya nchi hii.
Nafikiri
ni muda muafaka kwa nchi kwa chama kuangalia njia mpya za kusonga mbele.
Ni vizuri chama kikaanza kutafuta njia makini za kufanya Watanzania
waone upi ukweli na uwongo. Na ni muhimu sana kwa sasa Kambi rasmi ya
upinzani Bungeni itafakari mbinu za kufanya majibu ya msingi yatolewe
kuhusu hoja zilizoahirishwa tangu nyuma pamoja na hatua za kuchukuliwa
au kama kuna zilizochukuliwa wananchi wajulishwe.
NAAMINI
KUWA WOTE HATUTAPENDA KUONA MATOKEO YA KUPUUZWA kwani tutashindwa
kuwasadikisha waTanzania kuwa swala la mabadiliko ni muhimu na serious
kwa sasa.
Katika
harakati,
0 comments:
Post a Comment