Takwimu za
Jeshi la Polisi Tanzania
kitengo cha Usalama Barabarani kuhusu hali ya ajali za barabarani kwa
mwaka
2012 zilizopo kwenye ripoti ya haki za binadamu iliyozinduliwa mwaka huu
zinaonesha kuwa mwaka 2012 kulikuwa na ajali 11438 na ambazo
lilisababisha vifo
vya watu 4919.
Katika
takwimu hizo zinaonesha kuwa Mbeya kulikuwa
na ajali 617 waliokufa ni
309,Pwani ajali 1330 waliopoteza maisha ni 238,Kilimanjaro ajali 1502 na
kuua
watu 208,Morogoro watu 285 walipoteza maisha yao kutokana ajali
1599,Ambapo
mkoani Arusha kulikuwa na ajali 2136 ambazo zilisababisha vifo vya watu
192 na
Iringa kulitokea ajali 791 zilizopoteza maisha ya watu 195,Mwanza ajali
533 na
kuua watu 235,Dar es salaam ndio inaonekana kuongoza kwa kuwa na ajali
2930
zilizosababisha vifo vya watu 431.
Kwa upande
wa ajali zilizosababishwa na pikipiki ama bodaboda takwimu zinaonesha
zilisababisha vifo vya watu 695 kwa mwaka 2011 na mwaka 2012 watu 930
ambayo ni
tofauti ya watu 235 ambapo mwaka 2010 kulikuwa na vifo vya watu 647
zilizosababishwa na pikipiki ikiwa ni
tofauti ya watu 48 kwa mwaka 2010 na 2011.
Miongoni mwa
sababu za ajali hizo ni uzembe wa madreva na kutofuatwa kwa sheria za
usalama
barabarani
0 comments:
Post a Comment