Kikosi cha Zima moto na uokoaji cha
Halmashauri ya mji wa Njombe kwa kushirikiana na wananchi wakitoa mwili
wa Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Abdalah Mgambo
baada ya kutumbukia kwenye kisima hicho jana katika Uwanja wa ukumbi wa
Turbo Mjini Njombe.
Mwili wa Eng.Abdalah Mgambo ukionekana
kwa umbali kwenye gari la Polisi ukipelekwa hospitali Kibena kwenye
chumba cha kuhifadhia maiti.
Wa pili kushoto ni Mhandisi wa Maji
Halamshauri ya Mji wa Njombe Eng.Abdalah Mgambo enzi za uhai wake wakati
wa Kilele cha Wiki ya Maji March 22 mwaka huu katika kijiji cha
Igominyi.
Marehemu Abdalah Mgambo enzi
za Uhai wake akisoma taarifa ya Hali ya maji katika halmashauri ya Mji
wa Njombe mwezi machi 22 mwaka huu wakati wa kilele cha wiki ya Maji
Igominyi Njombe.
.............................................................
Taarifa toka eneo la Tukio zinasema kuwa
marehemu Abdalah Mgambo alikuwa katika Baa yake eneo la Ukumbi wa Turbo
Mjini Njombe kisha akamuaga mke wake kwamba anatoka nje kujipumzisha
kwenye gari lake majira ya Moja jioni jana April 30 akatoweka ghafla na
kisha Kadi yake ya Benki ya NMB Ilikutwa nje ya Kisima cha Maji
kilichopo katika uwanja wa Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
Akizungumza na Mtandao huu wa
www.gabrielkilamlya.blogspot.com eneo la Tukio mara baada ya kuuokoa
mwili wa Mhandisi huyo Afisa mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini Bwana
Donald Mng'ong'o amesema kuwa leo asubuhi amepata taarifa toka kwa mke
wa marehemu kuwa alitoweka ghafla na mara baada ya kuikuta kadi ya ATM
nje ya kisima cha maji ndipo wakachukua jitihada za kuanza kutafuta
kwenye kisima hicho kwa kushirikiana na kikosi cha Zima moto na Uokoaji
cha Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Bwana Mng'ong'o amesema kuwa majira ya
Tisa jioni mei mosi ndipo mwili wa marehemu umeokolewa na kuwahishwa
katika Hospitali ya Kibena Njombe.
0 comments:
Post a Comment