Monday, October 7, 2013

Profesa Tibaijuka achangia sh. mil. 46 ujenzi kanisa Katoliki Kitunda



WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amechanga sh. Mil. 46 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kitunda, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Profesa Tibaijuka aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, Rais wa Awamu ya Tatu, Wiliam Benjamin Mkapa ambaye hakuwepo katika harambee hiyo alichangia sh. Mil. moja katika ya sh. mil. 95 zilizochangwa.

Katika harambee hiyo ambayo jiwe la msingi liliwekwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Policarp Kardinali Pengo aliyewakilishwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padri Raymond Sabba, Profesa Profesa Tibaijuka alimsifu Askofu Pengo kuhamasisha ujenzi wa makanisa ya kisasa na kuongeza huduma za kiroho kwa waumini kufikia parokia 79 za Jimbo la Kuu la Dar es Salaam.

Waziri alisema Serikali inafarijika kuona watanzania wanaishi maisha yenye utulivu na kuwapongeza viongozi wa dini kuendelea kutoa huduma za kiroho kwa waumini wao.

Alisema miji mingi duniani imeendelea kutokana na wananchi wake kuwa na nidhamu na kuongeza kuwa ongezeko la ukuaji wa kasi wa miji mingi hapa nchini ni changamoto kwa wizara yake kuhakikisha upimaji unafanyika.

Kanisa la Kitunda litakalogharimu sh. Bil. 1.5 mpaka litakapokamilika katika risala yao iliyosomwa na katibu wa Baraza la Walei Parokia ya Kitunda, Bw. Simon Nguka ilisema wanakabiliwa na changamoto nyingi mojawapo ni urasimu wakati wanafuatilia hati miliki ya eneo la kanisa hilo.

Profesa Tibaijuka alisifu ukubwa wa kanisa hilo na ramani yao ya kisasa na kuahidi kuwa upimaji wa nyumba za wakazi wa eneo hilo utaanza karibuni na kuwaomba wanananchi watoe ushirikiano kazi hiyo itakapokuwa imeanza.

Alisema upimaji utakapoanza kama kuna nyumba za kuabudia zitakuwa zinahitajika kuongezewa eneo wananchi wa nyumba jirani watoe ushirikiano wa kupisha maeneo hayo.

Katika mahubiri ya Padri Sabba aliyeongoza ibada ya misa takatifu aliwaomba waumini wa Parokia ya Kitunda kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa kanisa hilo.

mwisho

0 comments:

Post a Comment